Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kundi la muziki “Maktaba ya Istanbul” kwa kutayarisha na kuchapisha picha mjongeo yenye anuani "Shahid Rahbarimiz” (Kiongozi wetu Shahidi), limewasilisha kazi ya kisanaa katika kumtukuza na kumheshimu kiongozi shahidi wa Iran, Hadhrat Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei.
Kazi hii ambayo imeambatana na maudhui ya kishujaa na kihisia, imejaribu kwa mtindo wa kimuziki kuonesha nafasi ya kiroho na jukumu la uongozi wake, na inalenga kufikisha ujumbe wa uaminifu na mapenzi ya wasanii wa Kituruki kwa shakhsia hii.
Kuchapishwa kwa klipu hii katika anga ya vyombo vya habari kunatazamwa kuwa ni uakisi wa uhusiano wa kitamaduni na kihisia kati ya sehemu ya wasanii wa Uturuki na mikondo ya kifikra na kiitikadi iliyopo nchini Iran.
Maoni yako